Siku moja baada ya klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji imsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta, January 30 ilishuka dimbani ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Cristal Arena kuikabili klabu ya Kortrijk.
Licha ya kuwa Samatta hakuwa kwenye kikosi, kwa sababu hakufanya mazoezi na timu, KRC Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na mshambuliaji mwenye asili ya Zaire Christian Kabasele dakika ya 21, hizi ni taarifa na mapokezi mema kwa Samatta ambaye ndio kwanza ametua Ubelgiji kuanza maisha yake ya soka.
Mchezo wa mwisho kabla ya ushindi dhidi ya Kortrijk, KRC Genk ilicheza dhidi ya Mechelen na kutoka sare ya goli 1-1, kwa sasa KRC Genk ipo nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi. KRC Genk watarudi uwanjani February 6 kucheza dhidi ya Mouscron-Peruwelz na huenda mchezo huo Mbwana Samatta akawepo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.