Club ya Singida United ambayo kwa sasa imekuwa ikidaiwa kutokuwa vizuri kiuchumi kiasi cha kutetemesha kikosi chao na baadhi ya wachezaji kuondoka, leo imetangaza good news baada ya kufanikisha kuwasajili wachezaji wanne kutoka timu ya taifa ya Zambia ya vijana chini ya umri wa miaka 23.
Singida imewasajili wachezaji hao kwa mikataba ya kuanzia miaka mitatu hadi minne lakini imemsajili pia mchezaji kutoka Liberia kwa mkongwe wa soka George Weah aliyewahi kushinda Ballon d’Or na sasa Rais wa nchi hiyo, AyoTV imeongea na mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga na amefunguka kuhusiana na usajili huo na tuhuma za kudaiwa hawalipi mishahara wachezaji.
.
“Tumefanya usajili kwenye dirisha dogo ambao umelenga kuimarisha kikosi mnaweza mkaona kuwa Singida United imekuwa na kikosi ambacho sio kina nguvu sana, leo tumefanikiwa kuwasajili wachezaji wanne wanaocheza U-23 ya Zambia ambapo tumewapata kupitia mawakala wetu pale Zambia”>>> Festo Sanga
.
“Hizi ni jitihada za club na jitihada za uongozi kuhakikisha Singida United inarejea katika ubora wake unaweza kuona kuna maswali mbona wachezaji wanaondoka wanadai maslahi yao wengine lakini bado mnasajili, niwaambie kitu kimoja ukitokea msiba haukwamishi shughuli zingine kuendelea hatuwezi kukosa bajeti ya kusajili tunayo na hata kulipa mishahara tunalipa”>>>Sanga
Watanzania waishio Afrika Kusini wamejipanga kuelekea Lesotho leo