Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amekasirishwa Sana na utendaji usio ridhisha kutoka kwa Mkurugenzi na wakuu wake wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.
Kukasirishwa huko kwa waziri Jafo kumetokana na kushindwa kukamilisha kituo cha afya kwa mwaka mzima Licha ya kupewa fedha zote tangu January 2018, kushindwa kukamilisha ujenzi wa jengo la ofisi ya halmashauri kwa zaidi ya miaka 2 licha ya kupokea fedha zote za ujenzi, kushindwa kukamilisha ujenzi wa nyumba 4 za watumishi licha ya kupokea fedha zote kwa zaidi ya mwaka mmoja, pamoja na kasi ndogo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Kutokana na hali hiyo waziri Jafo amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kufanya uhakiki fedha za miradi hiyo katika halmashauri hiyo ya Buhigwe ili kujiridhisha kama fedha hizo zipo au zimefanyiwa ubadhirifu wa aina yeyote.
Aidha, katika ziara hiyo Waziri Jafo amewataka TBA kukamilisha ujenzi wa ofisi ya halmashauri ndani ya mwenzi mmoja ili watumishi wasiendelee kuteseka kwa kukosa ofisi wakati serikali yao imesha peleka fedha zote za ujenzi wa ofisi hiyo toka mwanzoni mwa mwaka uliopita.
ULIIKOSA HII YA MAWAZIRI SITA WALIVYOREJESHA OPERESHENI YA KUWAONDOA WAKULIMA BASI ITAZAME HII VIDEO UJIONEE NA WALICHOZUNGUMZA