Leo March 6, 2018 Mahakama ya Afrika Mashariki Divisheni ya kwanza, imetupilia mbali maombi Madogo yaliyowasilishwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Burundi ya kutaka kusimamishwa kwa shughuli za Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) mpaka hapo kesi ya msingi itakapo anza kusikilizwa.
Uamuzi huo umetolewa leo March 6, 2018 na Jaji Kiongozi, Monica Mugenyi akisaidiana na Jaji Isaac Lenaola na Jaji Fakihi Jundu wa Mahakama ya Afrika Mashariki ,iliyopo jijini ARUSHA.
Awali Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Burundi iliwasilisha maombi mawili katika mahakama hiyo akitaka Spika wa Bunge hilo Martin Ngoga pamoja na Ofisi ya Spika asitambuliwe huku ombi lingine ni kutaka kuunganishwa katika kesi hiyo Mbunge wa Uganda Fred Mukasambije.
Bashe vs Godbless Lema “unafiki ni huu wako”
Moto wateketeza vibanda 673 Mbagala DSM
Bashe vs Godbless Lema “unafiki ni huu wako”