Ofisi ya Taifa ya Takwimu ‘NBS’ imetoa taarifa ya mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi June 2018 ambapo imeelezwa kuwa imepungua hadi kufikia asilimia 3.4 ikilinganishwa na asilimia 3.6 ilivyokuwa mwezi May 2018.
Aidha imeelezwa kuwa kwa takwimu hizo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi June 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi May 2018
Kupungua kwa mfumuko huo kumechangiwa na baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula ambazo ni Bia kwa asilimia 1.1, gharama za ukarabati wa vifaa vya umeme na viyoyozi kwa asilimia 1.8, gesi za kupikia majumbani kwa asilimia 5.6, majiko ya mkaa kwa asilimia 2.0 na gharama za mawasiliano kwa asilimia 2.6.