Bado wiki moja imesalia michuano ya SportPesa Super Cup 2019 iweze kuanza ambapo kama ilivyoripotiwa awali, michuano hiyo kwa mwaka huu itaendelea kuhusisha timu za mataifa ya Kenya na Tanzania kama ilivyo kawaida lakini Bingwa wa michuano hiyo atapata nafasi ya kucheza na Everton katika ardhi ya nchi yake.
Tayari ratiba ya michuano hiyo imetoka na tumezifahamu timu zote nane zitakazoshiriki michuano hiyo kwa mwaka 2019 nchini Tanzania kuanzia January 22 hadi January 27 katika viwanja vya CCM Kirumba Mwanza na uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, michuano hiyo itahusisha Simba, Yanga, Mbao FC pamoja na Singida United kutoka Tanzania na vigogo wa soka Gor Mahia, AFC Leopard, Bandari FC and Kariobangi Sharks kutoka Kenya.
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso amesema kwa kuwa mshirika rasmi, SuperSport imepata idhini ya kuonyesha michuano hiyo mubashara kupitia DStv. “Tunafurahi kuujulisha umma wa watanzania kuwa hamu yao ya kushuhudia michuano hii mubashara kupitia DStv sasa imepatia jibu, sasa watashuhudia burudani hii ya aina yake tena kuanzia kifurushi cha chini kabisa cha Bomba”
Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tanzania Tarimba Abbas amesema “Tangu kuanzishwa kwa michuano hii miaka mitatu iliyopita, mashindano haya yamekua moja ya mashindano makubwa na yanayopendwa sana kote Afrika Mashariki. Umaarufu huu unakuwa mkubwa zaidi hasa ukizingatia kuwa mshindi anapata fursa ya kucheza na timu maarufu ya Everton ya Uingereza”
Mshindi wa Kombe la SportPesa 2019 atajishindia USD 30,000 lakini cha muhimu zaidi ni fursa ya kucheza na timu ya Everton, moja ya timu maarufu kabisa za soka Uingereza. Mshindi wa pili atajinyakulia USD 10,000 wakati mshindi wa tatu atapata USD 7,500 na mshindi wa nne USD 5,000. Timu zote zitakazo tolewa robo fainali zitapata USD 2,500 kila moja.
Michuano ya Kombe la SportPesa ilianza rasmi mwaka 2017 katika michuano iliyofanyika hapa Tanzania ambapo mshindi – Gor Mahia alicheza na Everton hapa hapa Tanzania. Msimu wa pili wa mashindano hayo yalifanyika huko Nakuru Kenya mwaka jana na mshindi kwa mara ya pili Gor Mahia alikwenda kucheza na Everton huko Liverpool Uingereza mwezi Novemba.
Mpenja katangaza goli kabla ya kona kupigwa, ataomba kutotangaza game za timu yake