Mkongwe wa soka wa Argentina Diego Maradona baada ya kusikia kuwa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetangaza kuwa Mexico, USA na Canada wamepewa uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2026, ameeleza kusikitishwa kwake na maamuzi hayo.
Maradona amefunguka na kueleza kuwa nchini za Mexico na Amerika Kaskazini hazistahili kupewa uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2026, jan June 13 FIFA walitangaza kuwa nchi za USA, Mexico na Canada ambazo zinatokea bara la Amerika Kaskazini ndio watakuwa wenyeji wa fainali za Kombe la dunia baada ya miaka nane.
Mexico, USA na Canada watakuwa waenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kufanikiwa kupata kura 134 kati ya kura 210 na kuwashinda Morocco ambao wameambulia kura 65 pekee, Maradona hajafurahishwa na maamuzi hayo.
“Sijapenda nchini za Amerika Kaskazini kupewa uenyeji wa World Cup 2026, hakuna hisia kule Canada wanaweza kuwa vizuri katika mchezo wa kuteleza katika mabarafu wakati USA wao watataka kufanya matangazo ya dakika 25 mara nne kujitangaza, kwa upande wa Mexico hawastahili kwa sababu wameshinda game mbili tu”>>>Maradona
FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018