Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Real Madrid wamemponza kocha wa timu ya taifa ya Hispania

on

Siku moja baada ya club ya Real Madrid ya Hispania kumtangaza kocha wa timu ya taifa ya Hispania Julen Loptegui kuwa ndio atakuwa kocha wao mkuu baada ya fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi mambo yamekuwa tofauti.

Chama cha soka Hispania kimefikia maamuzi ya kumfuta kazi Julen Loptegui kutokana na kutangazwa mapema kwa kocha huyo kuwa atajiunga na Real Madrid, kitu ambacho hakijawafurahisha viongozi hao.

Chief wa chama cha soka Hispania Luis Rubiales ameoneshwa kukasirishwa na Julen kutangazwa mapema kuwa ataondoka Hispania, kipindi ambacho anaamini hata kama anaondoka  alipaswa akili yake kuiweka katika World Cup na hakukuwa na ulazima wa kutangazwa mapema.

Julen Loptegui nafukuzwa kazi baada ya kuiongoza timu ya taifa ya Hispania katika michezo 20, ameshinda michezo 14, sare michezo sita, hakuna mchezo ambao amepoteza, timu imefunga magoli 61 na kuruhusu magoli 13 pekee.

VIDEO: Alichozungumza MO Dewji kabla ya kutoa tuzo za MO Simba Awards 2018

Soma na hizi

Tupia Comments