Rais mteule wa Gambia ambaye alikimbilia Senegal kutokana na hali ya hatari Gambia baada ya Rais aliyeshindwa kwenye uchaguzi kugoma kuondoka madarakani, aliapishwa kwenye ubalozi wa Gambia kwenye nchi jirani ya Senegal.
Sasa inawezekana na wewe umejiuliza kama mimi, kisheria imekaaje pale ambapo Mgombea anaeaminika kushinda kwa kura anakimbilia nchi jirani na kwenda kula kiapo cha Urais huko? Mwanasheria wa kujitegemea Mtanzania Jebra Kambole anatusaidia kwa ufafanuzi.
Anasema ‘Katiba ya Gambia ya mwaka 1997 imeweka mambo mbalimbali, kwanza ibara ya nne ya katiba inaeleza kwamba katiba ndio sheria kuu, ibara ya 63 inasema Rais Mteule atashika nafasi ya kwa miaka mitano mpaka pale Rais mwingine atakula kiapo‘
‘Kula kiapo haijaeleza iko sehemu gani lakini kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibalozi zilizosainiwa Vienna 1961 zimeweka wazi, sehemu ubalozi ulipo ni taifa jingine…. mfano Ubalozi wa Tanzania kule Kenya ni sehemu ya Tanzania hivyo hata Ubalozi wa Gambia Senegal ni sehemu ya Gambia‘ – Jebra
‘Kwahiyo kuapishwa kwa Rais kwa eneo la nchi nyingine lakini ndani ya ubalozi ni sawasawa na kuapishwa ndani ya nchi yako vilevile na haitokua kinyume cha sheria kwasababu sheria za kimataifa zinaruhusu, ndio maana Watanzania waliopo Marekani wakifunga ndoa kwenye ubalozi wa Tanzania Marekani inatambulika kisheria kama imefungiwa Tanzania vile‘ – Jebra Kambole
ULIPITWA? Tazama hapa chini video ya kituo kipya cha kisasa cha Mabasi Morogoro, camera kila mahali..