Kwa kawaida shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA huwa na utaratibu wa kutoa tuzo kadhaa mwishoni mwa mwaka, baadhi ya tuzo ambazo hutolewa huwa ni tuzo ya goli bora la mwaka (Puskas Award), tuzo ambayo hupewa mchezaji aliyefunga, lakini pia hutolewa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Ballon d’Or, hii ni tuzo ambayo tumeizoea.
February 16 nimekutana na goli la faulo lililofungwa Malaysia, lakini mtandao wa 101greatgoals.com kwa namna lilivyo fungwa ndio maana 101greatgoals.com imetabiri kuwa hilo linaweza kutwaa tuzo ya goli bora la Dunia kwa mwaka 2016, goli hilo limefungwa katika mchezo kati ya Pulau Pinang dhidi ya Pahang na limefungwa na Faiz Subri mwenye umri wa miaka 28 kwa mpira wa faulo.
Hili ndio goli lenyewe mtu wangu lililofungwa kwa faulo
Cc @sukanstar pic.twitter.com/AeCWKS0aiL
— Fadhlan Abdul Aziz (@fadhlanaziz) February 16, 2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE