Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez ametangaza kuwa Ligi Kuu ya Hispania LaLiga 2019/20 itaendelea June 8 2020 baada ya kusimama kwa muda sababu ya Corona.
“Kwa kushirikiana na baraza la michezo taa za kijani zimewashwa kwa kwa ajili ya michezo ya mpira wa miguu kuendelea kuanzia June 8 (Hispania)”>>> Pedro Sanchez
Taarifa ya waziri Mkuu inakuja ikiwa ni siku moja imepita toka Umoja wa wachezaji soka wa Hispania (AFE) walipokutana Ijumaa hii kujadili namna ya kurejesha LaLiga June 12 wakati huu wa changamoto ya janga la Corona.
Kama utakuwa unakumbuka Vizuri Ligi Kuu ya Hispania ilisimama toka March 2020, mapema wikii hii Rais wa LaLiga Javier Tebas alieleza kuisubiri LaLiga kwa shauku ikirejea baada ya kusimama kwa miezi mitatu sasa.