Kutokana na ukuaji wa Teknolojia pamoja na kasi kubwa iliyopo Duniani kwenye soko la Ushindani na Ubunifu, kila siku tunaona ubunifu mkubwa sana ukigusa headlines za habari kubwa Duniani !!
Kulikuwa na magari yanayotumia mafuta, zimekuja gari zinazotumia na nishati nyingine ikiwemo gari za umeme.. ikaja stori kwamba badala ya kupokeza muda kuchaji gari, Uingereza wakaitambulisha teknolojia ya barabara zinazochaji gari za umeme… hiyo ni mfano tu wa stori za kukua kwa teknolojia kwenye kasi kubwa sana Duniani.
Ninalo Daraja la kioo toka China… Daraja limekamilika na lina urefu wa kama Mita 300 hivi ambazo kwa hesabu ya kawaida ni urefu wa viwanja vitatu vya mpira, yani kutoka goli mpaka goli alafu viwanja viwe vitatu !!
Unaambiwa kwamba upana wa kioo kilichotumika kwenye huu ujenzi kina kama Milimita 24 ambazo ni kama mara 25 ya upana wa kioo cha kawaida, kwa hiyo hakuna shaka kuhusu uimara na usalama wa Daraja lenyewe !!
Daraja hilo limejengwa kuunganisha sehemu ambayo ni juu ya Milima kwenye Hifadhi ya Shiniuzhai Park, ambayo iko kwenye Jimbo la Hunan, Kusini mwa China.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE