Aliyekua Director wa vipindi mbalimbali vya televisheni na Filamu George Tyson ambaye alifariki kwa ajali ya gari Mei 30 akiwa njiani kutokea Dodoma anategemewa kuagwa Jumatano June 05 kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam
Awino Felix ambaye ni mdogo wa Marehemu George Tyson amesema kuwa mazishi wanategemea kuyafanya Nairobi Kenya mara baada ya hatua za kuaga mwili hapa Dar es salaam kukamilika na anategemewa kuzikwa Jumamosi ya wiki ijayo.