Baada ya kusubiri kwa muda wa masaa kadhaa mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano ya Euro 2016 uliyokuwa unamuhusisha timu mwenyeji, usiku wa July 7 2016 timu ya taifa ya Ufaransa ambao ndio wenyeji walicheza dhidi ya Ujerumani katika uwanja wa Stade Velodrome.
Huu ni mchezo ambao timu zote mbili zilikuwa zinapewa nafasi ya kushinda mchezo, ila Ufaransa walikuwa wana rekodi ya kuifunga Ujerumani mara 13, kupoteza mara 10 na sare mara 5, hiyo ni takwimu kwa mujibu wa mechi zao 28 walizowahi kucheza toka March 5 1931.
#MillardAyoUPDATES #LiveMatch dk ya 46 #Germany 0-1 #France (#Griezmann 45′) #EURO2016 pic.twitter.com/VJPLkeM5x3
— millard ayo (@millardayo) July 7, 2016
Rekodi na uenyeji umefanikiwa kuisaidia Ufaransa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, ushindi ambao uliisaidia timu hiyo kutinga katika hatua ya fainali katika radhi yao, magoli yote ya Ufaransa yalifungwa na Antoine Griezmann dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 72, Ufaransa sasa watacheza na Ureno katika mchezo wa fainali.
#MillardAyoUPDATES #LiveMatch dk ya 85 #Germany 0-2 #France (#Griezmann 45′ 72′) #EURO2016 pic.twitter.com/DPiZquJ8vE
— millard ayo (@millardayo) July 7, 2016
GOLI LA MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1