Baada ya club ya Azam FC kutotaka kumruhusu nahodha wao Himid Mao aondoke katika club hiyo kwa muda mrefu, hatimae leo June 1 2018 zimetoka taarifa za uongozi wa club hiyo kumpa baraka Himid Mao za kwenda kucheza soka la kulipwa.
Himid Mao leo ametangazwa kuingia mkataba wa miaka mitatu na club ya Petrojet ya Misri, mkataba ambao utamfanya aitumikie club hiyo hadi mwaka 2021, hiyo inakuwa ni taarifa njema kwa Himid na mashabiki wake kwani ombi lake limekubaliwa baada kuomba kwa muda mrefu.
Kama huifahmu Petrojet FC ni club ambayo ilianzishwa na kampuni ya mafuta ya Misri (Egyptian Petroleum) mwaka 2000 na hadi sasa ina umri wa miaka 18, ilipanda kucheza Ligi Kuu Misri msimu wa 2006/2007.
Petrojet FC ni timu inayotumia uwanja wa Suez kama uwanja wake wa nyumbani wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 27000 waliokaa, uwanja wa Suez ulijengwa mwaka 1990, uwanja huo pia unatumiwa na club ya Asmant El-Suweis kama uwanja wao wa nyumbani.
VIDEO: Mazoezi binafsi ya Simon Msuva na mdogo wake wakati huu akiwa likizo