Umeisikiliza U Heard ya leo? Unajua leo Soudy kamtobolea nani?
Soudy Brown a.k.a Gossip Cop leo kamnasa mkali kutoka Kigoma, Baba Levo story ikiwa ni kuhusu msanii huyo kumtelekeza mke wake akiwa mjamzito maeneo ya Kijitonyama, Dar.
Baada ya Baba Levo kuulizwa kuhusu hilo amekana na kusema mke wake aliyekuwa mjamzito ameshajifungua mtoto wa kike.
Mahojiano hayo yaliishia hivi:-
Gossip Cop : “… Umesema tena anaitwa nani vile?..”
Baba Levo : “… Aaaah… suala la anaitwa nani hujamzaa wewe ndugu yangu.. sikupi jina…”
Gossip Cop :“…Hebu nimsikie kidogo hapo akilia hata ng’aa ngaa hapo…”
Baba Levo : “…. Ng’aa ng’aa we nd’o umemzaa..? Huyu mtoto ni wa kwangu mimi.. mi’ ndiyo naweza kuamua alie au asilie.. mimi na watoto wangu mtuache.. watoto ni wa kwangu.. familia ni za kwangu ..niacheni na watoto wangu au sio bwana..!”
Kama hukusikiliza U Heard hiyo bonyeza play hapa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook