Mgombea wa Urais mara nne nchini Uganda Kizza Besigye na Mbunge wa jimbo la Kyadondo Mashariki nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la Bobi Wine wameripotiwa kuunganisha nguvu pamoja ili kuleta upinzani mkubwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Museven na Chama chake cha NRM kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo 2021.
Viongozi hao wawili wa kambi mbili za upinzani nchini Uganda kwa pamoja wamekubaliana kuunganisha nguvu sambamba na kushawishi baadhi ya wanachama wa ndani ya chama cha Museven NRM ili kuungana nao kumpinga Museven asishinde katika uchaguzi mkuu wa Rais wa nchi hiyo 2021.
Bobi Wine ambaye anawakilisha People’s Power na Kizza Besigye kutokea People’s Govenment, mazungumzo ya wawili hao yanadaiwa kuwa yalianza May 3 2019 Magere nyumbani kwa Bobi Wine na kuonekana kuwa wameafikiana kwa pamoja kuunda upinzani imara ili Rais Museven hasisinde tena Urais, Bobi Wine na Besigye wanampinga Museven asiendele na Urais katika muhula ujao kwani ametawala nchi hiyo kama Rais kwa miaka 33.
Rais Museven September mwaka huu anatimiza miaka 75 na kwa mara ya kwanza aliingia madarakani kama Rais wa Uganda ilikuwa 1986, huku taarifa zikiripotiwa kuwa Rais huyo anao mpango wa kugombea tena nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa 2021 nchini Uganda, umoja ulioundwa na Besigye na Bobi Wine unaripotiwa utaleta ushindani wa kweli wa kisiasa katika taifa hilo.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania
u