Mshambuliaji wa Juventus aliyepo katika club ya Chelsea kwa mkopo Gonzalo Higuan amefikia maamuzi ya kutangaza rasmi kustaafu kucheza mechi za kimataifa kwa timu yake ya taifa ya Argentina, Higuan ametangaza maamuzi hayo wakati huu akiwa na umri wa miaka 31.
Imeripotiwa kuwa Higuan amefikia uamuzi huo kwa sababu zake binafsi za kifamilia, Higuan ambaye kwa sasa amekuwa na wakati mgumu na nafasi yake katika club, ametangaza kustaafu kuichezea Argentina akiwa ameitumikia katika michezo 75 na kufunga magoli 31.
Gonzalo Higuan alianza kuichezea timu ya taifa ya wakubwa ya Argentina toka 2009, mchezo wake wa mwisho kuichezea Argentina ulikuwa ni World Cup 2018 nchini Urusi ambapo alicheza dhidi ya Nigeria, game ambayo ilimalizika kwa Argentina kupata ushindi wa 2-1.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars