Michezo

Yanga wanaendelea kukusanya point tu, Simba wakiendelea na viporo vyao

on

Yanga SC leo walikuwa Uhuru kucheza game yao ya 34 ya Ligi Kuu ya nchini England dhidi ya Tanzania Prisons, Yanga ndio walikuwa wenyeji wa mchezo huo uliohudhuriwa na idadi ndogo ya mashabiki ukilinganisha na ilivyokuwa katika game dhidi ya Azam FC.

Yanga leo pamoja na kuwa inaongoza Ligi kwa tofauti kubwa ya michezo dhidi ya Simba SC ambao ni washindani wao wa karibu, wamedhihirisha kuwa Simba SC wanapaswa kuwa makini na kupata ushindi katika michezo yake yote ya viporo kwani wao wanafunga na kujiongezea point.

Leo Yanga imeifunga Tanzania Prisons kwa magoli 2-1, magoli yakifungwa na Tshitshimbi dakika ya 23 na Heritier Makambo dakika ya 66, huku Prisons wakifunga goli moja pekee kupitia kwa Ismail Kada dakika ya 32, Yanga wanaendelea kuwa kileleni kwa kufikia point 80 tofauti ya point 8 na michezo sita dhidi ya Simba SC waliopo nafasi ya pili kwa kuwa na point 72, Prisons nafasi ya 8 kwa kuwa na point 42.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments