Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Neymar amedaiwa kukwepa kuhudhuria utoaji wa tuzo za Ligue 1 na kwenda kula bata na muimbaji Rihanna.
Habari hizo zimeenea katika mitandao kufuatia kuonekana kwa picha ya pamoja kati ya Neymar na Rihanna wakiwa pamoja sehemu za starehe, picha hiyo ya Neymar na Rihanna aliipost Neymar instagram na kuandika maneno “Malkia na mwanamke mwenye nguvu”
Usiku huo alionekana Neymar na Rihanna ulikuwa ni usiku wa utoaji wa tuzo za Ligue 1 ambapo mchezaji mwenzake wa PSG Kyliane Mbappe ameshinda tuzo mbili za mchezaji bora wa Ligue 1 na mchezaji bora mdogo pia.
Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC