Siku ya Ijumaa walitembelea shule ya Msingi Taifa iiliyoko Temeke jijini Dar es Salaam ambapo wawakilishi wa StarTimes walikutana na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la 4 na 5 katika shule hiyo na kuwaeleza kuhusiana na lengo la ujio wao.
Mbali na kuzungumza na wanafunzi wawakilishi hao walitoa zawadi ya king’amuzi cha Dish kwa uongozi wa shule na zawadi kadha wa kadha kwa wanafunzi waliojibu vizuri maswali na wale wanaofanya vizuri darasani.
“Ugeni wenu umewapatia wanafunzi chachu ya kujifunza Zaidi kwani kama tunavyojua watoto wanapenda hujifunza Zaidi kwa kutazama kuliko kusikiliza. Lakini pia imetusaidia kujua wapi kuna tatizo na sisi tunaweza kuongeza nguvu katika kuwafundisha wanafunzi wetu,” >>> Mwl. Mkuu wa Shule ya Msingi Taifa Bi. Juliana Lubuva.
“Lakini pia tuwapatie changamoto StarTimes wongeze maudhui ya teknolojia Zaidi kupitia katuni kwa sababu watoto wanaelewa Zaidi itawpa msukumo wa kupenda masomo ya sayansi na kupanua uelewa wao.”
ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambayo wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao, Kampeni hii ya kutembelea mashule jijini Dar es Salaam itaendelea hadi mwisho wa mwezi wa tano itafikia jumla ya shule 7 katika Wilaya 3 za Mkoa wa Dar es Salaam.
“Hatuwezi kuruhusu wananchi wetu wateswe na baadhi ya Askari”-Waziri Masauni