Michezo

Simba SC wameanza kurejea, wakipata point 21 kazi wamemaliza TPL

on

Wekundu wa Msimbazi Simba SC baada ya ushindi wa goli la dakika za lala salama lililofungwa na Hassan Dilunga dhidi ya JKT Tanzania katika ushindi wa 1-0, game iliyochezwa uwanja wa Uhuru sasa wameanza kuonesha dalili zote kuwa kuna uwezekana wakawa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 mara mbili mfululizo.

Simba SC baada ya ushindi huo wamekuwa nafasi ya pili wakiwa na point 72 na wapinzani wao Yanga wakiongoza kwa tofauti ya point 5 (77), huku Yanga wao wakiwa wamecheza michezo 33 wamebakiza michezo mitano, Simba SC wakiwa wamecheza michezo 28 na wamebakiza michezo 10 pamoja na game zao za viporo.

Kimsingi Yanga hadi sasa anatafuta point 15 wakati Simba SC anawania point 30, Yanga kama atashinda michezo yake yote mitano atapata point 15 hivyo atamaliza Ligi akiwa na jumla ya point 92, wakati Simba SC akishinda game zote 10 atamaliza Ligi akiwa na point 102, hivyo Simba anahitaji ushindi katika game 7 (Point 21) pasipo kujali matokeo ya timu yoyote ili awe Bingwa kwani atakuwa ana point 93 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments