Rais wa shirikisho la soka Afrika CAF Ahmad Ahmad mwaka 2018 alitembelea Tanzania na kushuhudia ugawaji wa tuzo za Ndondo Cup 2018 baada ya kumalizika kwa michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka la mchangani kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
Baada ya Ahmad Ahmad kufuatilia mwenendo wa mashindano hayo pamoja na ugawaji wa tuzo za mashindano hayo kwa wachezaji, waamuzi na shabiki aliyefanya vizuri, aliipongeza Clouds Media Group pamoja na kampuni ya Shadaka Sports Management kwa uandaaji wa mashindano hayo huku akiahidi kutoa mipira 50 kama zawadi na kusapoti mashindano hayo.
Akiwa Tanzania katika fainali za michuano ya maifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON U-17 2019), Ahmad Ahmad amekabidhi mipira hiyo kama alivyoahidi kwa mwenyekiti wa kamati ya michuano hiyo Shaffih Dauda, tukio hilo lilishuhudiwa pia na Rais wa TFF Wallace Karia.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania