Shirikisho la soka Tanzania TFF March 15 lilitangaza adhabu ya kumfungia maisha kujihusisha na soka makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu, moja kupokea pesa za TFF isivyo halali, kugushi na kushusha hadhi ya TFF.
Baada ya kushindwa rufaa leo Wambura akiwa na Mwanaseheria wake Emmanuel Muga ameongea na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha TFF hukumu ya Mahakama Kuu ya kutengua maamuzi hayo kutokana na kugundua kuwa kumekiukwa baadhi ya taratibu katika kufanywa maamuzi hayo, leo ni siku ya 265 toka TFF itangaze kumfungia maisha Wambra.
“Tumekuja hapa kukabidhi maamuzi ya Mahakama Kuu Tanzania ya kupinga maamuzi ya kamati za TFF, mwezi uliopita Mahakama Kuu ilitengua maamuzi ya mimi kufungiwa kushiriki soka kwa maana hiyo baada ya maamuzi yale tarehe 30 naendelea kuwa Makamu wa Rais wa TFF”>>>Michael Wambura
Alichozungumza mwanasheria wa Wambura baada ya kushindwa rufaa