Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi baada ya kufunga goli lake la pili katika AFCON 2019 akiwa na timu yake ya Uganda akicheza dhidi ya Zimbabwe, ameeleza namna ya timu yake ilivyopiga hatua kwa haraka katika michuano hiyo baada ya kushirikia AFCON 2017.
Okwi ameeleza kilichopeleka au kinachosababisha sasa hivi wafanye vizuri ni kutokana na wachezaji wa Uganda wanafahamu kuwa wanacheza na watu waliokuwa na uwezo wa juu, hivyo njia pekee ya wao kuwa na uwezo wa kupata matokeo na kupamba na timu hizo ni kucheza na kushindana nao kama timu.
“Siri yetu ya mafanikio sisi ni kwamba tunapambana kwa pamoja, tunacheza kwa pamoja na tunafanya kazi kwa pamoja, sisi hatuna staa katika timu kwa sababu tunajua hatujalingana na timu zingine, sasa sisi kazi yetu ni kuhakikisha tunapambana na tusivunje team spirit na team work”>>> Okwi
VIDEO: Inabidi Muielewe tu Taifa Stars, Msuva Kaongea Kwa Hisia