Simba SC ambao ndio Mabingwa watetezi wa michuano hiyo wameanza kwa kishindo kwa kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1, magoli ambayo yalifungwa na Meddie Kagere dakika ya 3 na 58 kabla ya Miraji Athumani kufunga goli la mwisho dakika ya 73, baada ya mchezo huo kocha wa Simba SC Patrick Aussems aliongea na waandishi wa habari.
“Kabla ya mchezo tulijua kabisa itakuwa ngumu tumeathirika wiki hii kwa sababu tumetolewa Ligi ya Mabingwa ila wachezaji wameanza vizuri na kujaribu kufunga kadri iwezekanavyo na ndani ya dakika 15 tukafunga, baada ya kucheza kidogo tukiwa comfortable na kipindi cha pili tukafunga lakini nilikasirishwa dakika 15 za mwisho tulitakiwa tufunge goli la nne hata la tano lakini badala yake tukacheza kama watoto na kuruhusu goli”>>>>Aussems
VIDEO: Zahera katoa povu “Mpango wa kukwamisha Yanga haujaanza leo”