Maajabu

Pale ambapo mtoto anachukua bastola na kuwapiga wazazi wake…

on

boy yrs

Wazazi wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanalinda watoto wao kila wakati ili waweze kuwa salama ikiwa ni pamoja na kuwaweka kwenye mazingira mazuri.

Lakini wazazi wa mtoto huyu wamejikuta wakiwa hoi hospitali baada ya mtoto wao wa miaka mitatu katika mji wa New Mexico kuchukua bastola iliyokua ndani ya mkoba wa mama yake na kuwafyatulia wazazi wake.

Justin Reymond ambaye ni Baba wa mtoto huyo alipigwa risasi ya sehemu ya mgongo huku mama yake, Gabrielle Burkhart ambaye ni mjamzito wa miezi nane naye akijeruhiwa vibaya katika bega lake.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments