Mix

Video hii ni ushuhuda wa tukio la mauaji ya mtu mwingine mweusi Marekani

on

police-lineNi kama dunia ilianza kusahau matukio ya ubaguzi wa rangi, ishu ikarudi kuanza kuzungumziwa tena mwaka 2014 baada ya matukio ya watu wawili kuuawa mfululizo na Askari Marekani.

Leo hii ni story ya Afisa mwingine wa Polisi wa jimbo la CarolinaKusini kushtakiwa kwa mauaji, ushahidi wa video unaonesha Askari huyo alimpiga risasi nane mgongoni mtu ambae ni Mmarekani  mweusi.

Walter-Scott-2-600x313

Marehemu Walter Scott

Tukio hilo limetokea Jumamosi April 4 2015 ambapo shahidi mmoja alirekodi tukio hilo kwa video inayomuonesha Marehemu Walter Scott ambaye umri wake ni miaka 5o akikimbizwa na Afisa wa Polisi mzungu aliyekuwa na bunduki, akampiga risasi nane mgongoni, Walter alipoanguka alimfunga pingu.

screen-shot-2015-04-07-at-3-43-02-pm

Walter Scott akimkimbia Polisi

Afisa huyo Thomas Slager amejitetea kuwa Mmarekani huyo mweusi alikuwa akiendesha gari, alipomsimamisha kwa ajili ya kukaguliwa, alionekana kupingana na amri ya Polisi, akamuibia Polisi kifaa chake ambacho huwa Askarii wanakitumia kuwapiga shoti ya umeme wahalifu, Askari huyo akaamua kumpiga risasi.

scw

Walter Scott akifungwa pingu na Polisi

Hata hivyo Thomas Slager ameshtakiwa kwa mauaji na anakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha miaka 30 jela.

ws_21d713ac97c0ce379d3b23a3adcae87d

Thomas Slager akipandishwa kizimbani

Tazama video ya tukio hilo kwa kubonyeza play hapa chini…

millardayo.com ni sehemu yako utakapozipata zote unazozitaka, vichekesho, stori za siasa, muziki, michezo, movies, magazeti, video mpya na nyingine kubwa….  unaweza kujiunga na mimi Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments