Mei 4 2016 Bunge limeendelea Dodoma ikiwa ni mkutano wa tatu, kikao cha kumi na mbili ambapo katika kipindi cha maswali na majibu Mbunge Mgeni Jadi Kadika viti maalum aliulizwa swali kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Swali lake lilikuwa ni…>>>’Ugonjwa wa Myoma ni moja kati ya matatizo makubwa yanayoathiri akina mama kuzuia uzazi na kusababisha kansa ya kizazi pamoja na kupoteza maisha.’
‘Je, ni kwa kiasi gani Serikali imefanikiwa katika kuwasaidia akina mama wanaoteseka na matatizo haya?’
Majibu yakatoewa na Naibu Waziri Hamisi Kigwangalla…>>>’Myoma au kwa jina la kitaalamu unajulikana kama ‘Uterine Fibroid’ ni uvimbe unaoota kwenye misuli ya tumbo la uzazi wa mwanamke.’
‘Chanzo halisi cha Myoma hakijulikani ila kila Myoma huanza kwa ukuaji hovyo wa seli moja, ambayo hutoa protini kwa wingi. Tafiti pia zimeonyesha Myoma hutokana na mabadiliko ya vinasaba kwenye seli za Myoma ambazo hubadilisha ukuaji wa seli hizo.’
‘Myoma ni uvimbe ambao siyo Saratani, na hauna tabia ya kubadilika kuwa saratani. Myoma ikiwa kubwa huweza kuonyesha dalili kama kuvimba tumbo, kuvuja damu kwa wingi na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu‘
‘Serikali huwahamasisha wakina mama wote kupima afya zao kabla ya kushika ujauzito, wakati wa ujauzito hata baadaya kujifungua. Japokuwa siku hizi kuna dawa ambazo daktari anaweza kumpatia mama kabla ya uvimbe kuwa mkubwa‘
‘Aidha, kama uvimbe umekaa sehemu ambayo haufai kutolewa wenyewe na mamaa amekwishamaliza kuzaa basi hushauriwa kutoa mfuko wa kizazi (uterus)‘
ULIIKOSA HII UNASHAURIWA KUFANYA HAYA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA ILI KUEPUKA MAGONJWA?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE