Kila mwaka jijini Arusha hufanyika Bonanza la Pasaka la kimataifa la Kitambi Noma, ambapo kwa mwaka huu litatimua vumbi kwa siku mbili, Maandalizi kuelekea bonanza la michezo la kimataifa la Kitambi noma imeendelea kushika kasi jijini Arusha, michuano hii inalenga kukimbizana na magonjwa kama kisukari na hata kuondoa kitambi kwa kufanya mazoezi.
Jumla ya timu tisa za Maveterani kutoka Tanzania na Kenya zimethibitisha kuwa zitashiriki huku kwa mwaka huu zikitarajiwa kutoana jasho katika bonanza hilo, ambalo limezidi kuwa na mvuto mwaka hadi mwaka, umaarufu wa Bonanza hilo unakuja kutokana na jina la ‘Kitambi Noma’.
Bonanza hilo ambalo hufanyika kila mwaka kipindi cha siku kuu ya Pasaka kwa kuandaliwa na club ya maveterani ya Kitambi Noma ya jijini Arusha, mwaka huu limepewa jina la “KITAMBI NOMA UTALII INTERNATIONAL BONANZA” ikiwa na lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya jiji la Arusha na kuunga mkono juhudi za Mkoa huo kutangaza utalii nchini .
Bonanza hilo litafanyika kwa siku mbili kesho Jumamosi April 20 na 21 siku ya Jumapili katika uwanja wa General Tyres kwa kushirikisha timu tisa tatu kutoka jijini Nairobi nchini Kenya na sita kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Ruvuma na wenyeji Arusha.
Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23