Moja kati ya maswali yanalota ubishani mkubwa kwa mashabiki mbalimbali wa soka duniani ni pamoja na ulinganisha wa wachezaji wakongwe wa zamani na wasasa ni wapi walikuwa bora kwa nyakati zao, kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson ameweka wazi msimamo wake kuhusiana na suala na Diego Maradona na Lionel Messi nani bora.
Ubishi huu ulikuwepo katika ya mwanishi wa habari za michezo marehemu Hugh McIlvanney aliyefariki January 24 2019 dhidi ya mchambuzi na mchezaji wa zamani wa Liverpool Graeme James Souness, Hugh McIlvanney alikuwa anaamini Maradona ni bora dhidi ya Messi.
Wakati Graeme James Souness anaamini Messi ni bora zaidi ya mkongwe huyo wa Argentina Diego Maradona, swali lilipomfikia Ferguson jibu lake limetofautiana na marehemu swahiba wake Hugh McIlvanney kwa kuwa yeye amemtaja kuwa Messi ni bora zaidi ya Maradona kwa sababu Messi amekaa katika kiwango cha juu kwa miaka miwingi.
“Kwa hilo naungana na Graeme Souness kuwa Messi ni bora zaidi ya Maradona, kwa sababu wakati Maradona anacheza soka alikaa katika kiwago cha juu kwa miaka michache ukilinganisha na Lionel Messi ambaye amecheza kwa kiwango cha juu miaka mingi” >>> Sir Ferguson
Maradona ameshinda makombe 8 pamoja na Kombe la Dunia, mchezaji bora wa karne na ameitumikia Argentina katika game za timu ya taifa 91 akipachika magoli 34, huku Lionel Messi akiwa na rekodi ya kutwaa mataji 22 akiwa na FC Barcelona na kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina katika game 128 na kuifungia magoli 65 bila kusahahu ushindi wa tuzo ya Ballon d’Or mara tano.
Haji Manara katolea ufafanuzi tuhuma za kuita washabiki wapumbavu