Moja ya stori ya kuifahamu leo March 18, 2018 ni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia Dr. John Magufuli kumrudishia Prof. Costa Mahalu hadhi yake ya ubalozi ikiwa ni miaka takribani 11 tangu avuliwe hadhi hiyo.
Prof. Mahalu alivuliwa hadhi ya ubalozi mwaka 2007 baada ya kufunguliwa mashtaka ya jinai na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo mwaka 2012, mahakama ilitoa hukumu kwamba Prof. Mahalu hakuwa na hatia.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje inasema “Kuanzia leo tarehe 17/3/2018, Prof. Mahalu ataendelea kuwa na heshima ya kuitwa balozi,” .