Mwanasheria wa Kujitegemea, Leornad Manyama amezungumzia sheria ya kanuni za adhabu kuhusu watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga, ambapo amesema ni kosa la jinai kwa mtu kushiriki tendo la ndoa kinyume na maumbile ama na mnyama.
Mwansheria Manyama amesema kwa mujibu wa kifungu cha 154 cha Sheri za Kanuni za Adhabu inasema ni kosa la jinai ambapo inazuia mwanauem kuwa na mahusiano na mwanaume mwenzake, ama mwanaume na mwanamke kinyume na maumbile.
“Mtu akithibitishwa mahakamani ametenda kosa la namna hiyo, adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 14 jela, hivyo mtu anayejihusisha na vitendo hivyo anakuwa ametenda kosa la jinai,”amesema Manyama.