Serikali imekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya mitandao ya kijamii zinazosema kuwa watu 92 wamekufa mkoani kwa corona katika kipindi cha wiki moja iliyopita na kuzikwa kwenye makaburi ya Kola yaliyopo katika manispaa ya Morogoro
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi mkoani hapa mara baada ya kutembelea eneo hilo la makaburi na kufanya uchunguzi wa kuyaona makaburi hayo kama yanavyotangazwa
“Kumekuwepo na taarifa zinazoashiria matumizi yasiyo sahihi ya kimtandao na hivyo kuleta taharuki kwa wakazi wa Morogoro,imefika hapa nijionee mwenyewe makaburi hayo 92,sijayaona hayo makaburi yaliyosemwa” Prof. Makubi
Katika ziara hiyo Prof. Makubi aliweza kutembelea sehemu zote za makaburi hapo Kola , ikiwa pia kupata taarifa toka kwa vijana wachimba makaburi ambao wamekuwepo hapo zaidi ya mwaka.
Aidha, Mganga Mkuu wa Serikali, aliwaasa baadhi ya wananchi kuacha kupotosha jamii kwa taarifa za uongo kama kwamba wao wanafurahia vifo.