Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Makondo ameagiza halmashauri zote na Mikoa kutenga Fedha katika bajeti zao ili kutekeleza mpango wa Usajili wa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano kupata vyeti vya kuzaliwa ambapo jukumu la halmashauri kwa mujibu.
Akizungumza katika kikao cha kufanya tathimini katika zoezi la usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka amesema tayari wizara imetoa maelekezo kwa RITA kushirikiana na wataalamu wa Wizara kuandaa mpango mkakati ili kuwafikia watoto wenye chini ya miaka 5 ambao bado hawajafikiwa katika hatua za awali katika Mpango wa Usajili.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ameziagiza halmashauri (7) za mkoa huo, kuwasaka watoto wenye chini ya miaka 5 ambao hawajafikiwa na zoezi la usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwani ni muhimu serikali kupata takwimu sahihi za vizazi na vifo.