Mtayarishaji wa Muziki nchini Master Jay ambaye ni mmiliki wa MJ Records amezungumzia kuhusiana na tasnia ya muziki kiumjla ikiwalenga Watayarishaji pamoja na wasanii ikiwemo mauzo ya muziki pamoja na utofauti wa kipato kilichokuwa kikipatika miaka ya nyuma na sasa.
Kupitia mahojiano aliyoyafanya Master Jay leo April 18,2019 kupita kipindi cha XXL cha Clouds FM amegusia kuhusu urafiki wake na producer mwenzake P Funk Majani na kuzungumzia vingi ambavyo Watanzania hawakuvifahamu wakati huo. Hayo ndio baadhi ya mambo aliyozungumza Master Jay kupitia Clouds FM leo.
“Mimi na P Funk Majani tulitoka pamoja kwenye game na nakumbuka kabla yetu kulikuwa na BonLovw ambaye ndiyo alikuwa anafanya vizuri na sisi tulikuwa tunamuangalia sana yeye na nakumbuka sisi yaani mimi na P Funk tulikuwa tunataka kumuona tu, Watu hawajui kuwa mimi na Majani ni marafiki wa muda mrefu sana na hata kwenye ndoa yangu ya kwanza yeye alikuwa best man, sema soko la muziki likakolea na hela zikaingia kati”
“ Soko la Muziki lilianza baada ya Clouds FM kuanza na nakumbuka Joseph Kusaga pamoja na marehemu Ruge Mutahaba walikuwa wanatembea kila studio kutuambia turekodi kazi zetu kwa njia ya digital ili wao waweze kuzitangaza, BigUp kwa Clouds kwa hilo”
“Kipindi cha nyuma nilishawahi kufanya kazi na Wagosi wa Kaya na nakumbuka tulikuwa tunapiga hela nyingi sana kipindi hicho na niliwaambia jengeni na kiukweli hawakujenga maana niliuliza gharama za kujenga nyumba na walisema million 40, lakini matokeo yake waliuliza gari yangu ya BMW nilinunua shs ngapi nikawatajia bei na jioni wakaja na hiyo hela na kuchukua gari”
“Wakati natengeneza music, kuna wasanii walikuwa wanalipwa mpaka mil 100 in Advance kabla hata album haijauzwa kutoka kwa Distributors. Kati ya wasanii ambao nakumbuka tulipiga hela ni wagosi wa Kaya”
AUDIO: Ulipitwa na mwigizaji Irene Uwoya kutema cheche “Kuna watu nikuwafungia vioo tu”? Bonyeza PLAY hapa chini kusikiliza