Stori kubwa ambayo ime-trend siku ya leo July 15,2019 ni kuhusu video clip ikumuonyesha muigizaji Irene Uwoya akiwatunza waandishi wa habari na wakaonekana wakigombania pesa hizo mashabiki wameenda mbali na kila mmoja kutoa maoni yake kuhusu hilo.
Kupitia ukuarasa wa instagram wa Irene Uwoya ameamua kuwaomba radhi waandishi wa habari na kusema kuwa hakufanya hivyo kwa lengo la kuwadhalilisha kama ilivyotafsiriwa amesisitiza kuwa alifanya kwa moyo mzuri kutokana na juhudi za waandishi wa habari kwenye kusambaza taarifa.
“Ndugu zangu waandishi wa habari, leo katika press conference ya Swahili Inflix na ndugu zetu waandishi wa habari niliamua kutoa fedha kwa style ya kutunza.Baadhi yenu mmekwazika kwa kitendo hicho nawaomba radhi sana sikuwa na nia mbaya juu yenu, binafsi nawapenda waandishi wa habari kwani nyie ni watu muhimu sana katika jamii”
“Sikufanya hivyo kwa lengo la kuwadhalilisha kama ilivyotafsiriwa.Kama binadamu moyo wangu ulijawa na upendo na furaha iliyopitiliza ndipo niliona niweze kushiriki nanyi furaha hiyo kwa aina ile ya kuwatunza pesa,sababu mara nyingi mmekuwa watu muhimu katika kazi na mambo yote yanayohusu sanaa yetu na jamii kwa ujumla”
“Na baadhi ya waandishi ambao kwa bahati mbaya waliharibu vifaa vyao wakati wa kuokota shukrani yangu hiyo(pesa) naomba mniwie radhi na mnisamehe sana na poleni sana kwa changamoto.Pia kuhusu ndugu zangu waandishi kuwaomba kuvaa suti ile nilikuwa na maana nzuri ya kwamba katika utanashati wenu wa kila siku sisi tulipendelea siku ya tar 31st August katika show yetu inayoandaliwa na”
“Swahili Infilix itakayokuja kuleta mapinduzi makubwa na ukuaji mkubwa zaidi wa filamu zetu za hapa nyumbani tunatamani kuona wote mkiwa katika uniform ambayo itawatambulisha vyema kimavazi ambayo kwa wazo letu tuliweka suti na kiukweli mtapendeza sana na zaidi ya kawaida tulivyozoeana.”
“Nawapenda sana maana hakuna mimi bila nyinyi nathamini na kuwashukuru sana sana.Na zaidi naomba radhi kwa yeyote aliyekwazika kwa namna moja au tofauti.
Asanteni sana”
ULIPITWA NA HII VIDEO YA UWOYA AMWAGA PESA KWA WAANDISHI, AVURUGA MKUTANO? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA