AyoTV na millardayo.com inakukutanisha na historia ya eneo la ‘Maji Matakatifu’ ambalo lipo katika Hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo, unaambiwa Wazinza huwa wanakuja kwenye eneo hili kwa ajili ya kuomba ufumbuzi wa mambo mbalimbali yanayowatatiza kwenye maisha yao ikiwemo akina Mama kuchelewa kupata Watoto na wanaoga maji hayo huku wakitoa fedha (sarafu) huku wakielezea matatizo yao na yanatatuliwa.
Kwa sasa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA )wameligeuza eneo hili kama fursa na kulifanya kuwa eneo la Utalii.
SUMAYE, MBOWE WATAJWA UENYEKITI CHADEMA TAIFA, TUNDU LISSU AACHIWA NA KUBENEA