Moja kati ya habari ya kushangaza ni hii kutokea nchini Marekani (USA), Mwanamke kushika ujauzito kwa miezi tisa bila kugundua kuwa ni mjamzito imewashangaza wengi.
Tukio hilo limetokea Tennessee US baada ya mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Lauren Chalk kushika ujauzito na kutotambua hadi zilipofika siku 9 kabla ya kujifungua ndio akabaini kuwa yeye ni mjamzito baada ya mama yake kuhisi binti yake mjamzito na kumpeleka kupima.
“Nikikupa stori ya kuharibika kwa ujauzito niliyopitia, nisingeweza kuhisi kama mimi ni mjamzito ningepima kipimo cha mimba na najua kingeonesha mjamzito ningefikiria hiyo sio kweli” >>>Lauren Chalk
Lauren ,28, alikuwa hatarajii hilo kutokana na kuwa na tatizo la kuharibika kwa ujauzito mara kwa mara pale anapokuwa ameupata, iliwahi kumtokea hivyo 2014 na 2016 lakini December 2 2019 amefanikiwa kupata mtoto wa kiume na kumpa jina la Wyatt.