Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amelieleza Bunge kuhusu wananchi wake wanavyopata changamoto katika sekta ya afya kwa kukosa vituo vya afya vya kutosha pamoja na madaktari lakini bado wanasikia kwamba kuna Trilion 1.5 hazieleweki zilipo ambazo zingeweza kusaidia kupunguza changamoto zao.
“Serikali bado ina upungufu wa vituo vya afya kwa ajili ya kuwasaidia wananchi ikiwemo katika jimbo la Mikumi, Wilaya yetu ya Kilosa tuna upungufu pia wa madaktari mngetudondoshea madaktari ingetusaidia ”
“Lakini pia madawa yamekuwa machache na unaposikia Trilion 1.5 hazieleweki zimekwenda wapi nafikiri zingeweza kupangiwa mkakati maalum katika sekta ya afya na zikawasaidia watanzania” –Professor Jay
Majibu ya Serikali kuhusu kutoonekana kwa Trilion 1.5