Ligi kuu ya England inafahamika kwa jinsi ilivyo mahiri kwa matumizi ya nguvu na kasi hali ambayo hulazimu wachezaji wanaocheza ligi hii kuhakikisha wanazoea mazingira yake na mara nyingi wengi hushindwa kumudu mikimiki yake na kurudi walikotoka .
Moja kati ya watu ambao wanaweza wakaelezea dhana hii kwa ufasaha kuliko wote ni nyota wa Chelsea Eden Hazard ambaye ametajwa kuwa mchezaji ambaye amechezewa rafu kuliko wachezaji wote kwenye ligi hii .
Katika hali ya kawaida mtindo wa uchezaji wa Hazard unalazimu mabeki na viungo wakabaji wa timu pinzani kumchezea rafu kwani ni mchezaji mwenye kupenda sana kumiliki mpira huku akiwahadaa mabeki na wachezaji wengine wa timu pinzani kwa chenga zake za maudhi .
Eden Hazard amechewa rafu na wachezaji wa timu pinzani mara 74 , kiwango ambacho ni kikubwa kuliko vyote ka wachezaji waliochezea rafu toka timu mbalimbali katika mechi za ligi ya England .
Katika orodha hii nafasi ya pili imekwenda kwa Raheem Sterling ambaye amechezewa rafu mara 60 na ukitazama uchezaji wa Raheem Sterling ambaye kasi yake na ujanja wa kumiliki mpira na kuwapita mabeki unawaachia wapinzani wazo moja tu la kumzuia nalo ni kumchezea rafu unaweza ukaelewa kwanini anaingia kwenye orodha hii .
Mshambuliaji wa Everton Steven Naismith na Kiungo mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez wameingia kwenye orodha hii wakiwa kwenye nafasi ya 3 na ya 4 ambapo wamechewa rafu mara 52 na mara 47 katika mpangilio .
WACHEZAJI WALIOCHEZEWA RAFU NYINGI EPL (2014/15)
Mchezaji Idadi ya Rafu.
Hazard, Eden 74
Sterling, Raheem 60
Naismith, Steven 52
Sánchez, Alexis 47
Agbonlahor, Gabriel 46
Cabella, Rémy 45
Fer, Leroy 45
Sessegnon, Stéphane 44
Colback, Jack 44
Wickham, Connor 41
Cazorla, Santiago 41
Mané, Sadio 41
Song, Alexandre 40