Michezo

Mkataba wa Hazard ni ‘ndoa ya muda mrefu’ ndani ya Chelsea

on

hazzzz

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard hii leo ( alhamis) ametia saini mkataba mpya ndani ya klabu yake utakaomfanya abakie Stamford Bridge mpaka mwaka 2020 wakati mkataba huo utakapokwisha.

Mchezaji huyu raia wa Ubelgiji ambaye alisajiliwa na Chelsea akitokea nchini Ufaransa kwenye klabu ya Lille Metropole amekuwa moja kati ya wachezaji bora kwenye ligi ya England tangu aliposajiliwa na kwenye kila mechi amekuwa akionyesha umuhimu wake.

Katika mkataba huo Hazard atakuwa analipwa paundi 200,000 na anakuwa mchezaji wa kwanza kutia saini mkataba mpya na klabu yake tangu kuwekwa wazi kwa mkataba mpya wa haki za matangazo ya televisheni wenye thamani ya mabilioni ya pauni.

Hazard akitia saini mkataba mpya Chelsea .

Hazard akitia saini mkataba mpya Chelsea.

Tangu alipojiunga na Chelsea, Hazard amejijengea hadhi kama moja kati ya wachezaji wanaogopwa na mabeki wa timu pinzani hali ambayo imefanya kusaini kwake kuwa ushindi kwa Chelsea.

Tayari Hazard alianza kuhusishwa na harakati za usajili kwenda klabu kubwa barani Ulaya ikiwemo Real Madrid ambayo imekuwa na kawaida ya kusajili wachezaji nyota toka klabu mbalimbali barani Ulaya.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments