Star wa singo ya Mpenzi Bubu H baba leo ametoa picha kadhaa ambazo zinatambulisha ujio wa video na singo yake mpya inayoitwa Tubebane ambayo ndani yake kuna sauti ya msanii mpya anayeitwa Melon.
Video hii yote imefanyika Mwanza sehemu tofauti kama Salma Corn pamoja na Capripoint,ukiangalia kwenye hizi picha kwa mbaali utaona mandhari ya ziwa Victoria,exclusive interview na millardayo.com H Baba kasema sababu kubwa ya yeye kufanyia video Mwanza ni sababu amefanya video nyingi nje ya Mwanza sasa ni zamu ya Mwanza kwa sasa.
Hizi ni baadhi ya picha hizo zitakazoonekana kwa video mpya ya H baba.