Kama hukupata time ya kutazama Taarifa ya Habari kupitia TV za Tanzania April 7 2016 millardayo.com inakupatia fursa ya kutazama habari 5 kubwa zilizosomwa kwenye TV za Tanzania.
Habari kutoka Channel 10…Mazingira Duni Shule ya Ipuli Tabora
Wanafunzi katika shule ya msingi ya Ipuli iliyopo Manispaa ya Tabora wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko baada ya shule iyo kujaa maji kufuatia mvua inayoendelea kunyesha. ‘Hali ya hapa ni mbaya ukiangalia kipindupindu kimetoka siku za karibuni ni vyema kama hawatachukua hatua za haraka ni bora shule ifungwe‘>>>Mkazi
Habari kutoka Channel 10…TRA yakamata Bidhaa Wilayani Kilwa
Mamlaka ya mapato nchini ikishirikiana na jeshi la polisi limefanikiwa kukamata bidhaa mbalimbali za matumizi ya binadamu zilizoingizwa nchini kupitia njia za panya, ‘Kwa kweli ni changamoto ambayo hinaitaji msaada wa wananchi, na Jeshi la Polisi na niseme tu kuwa mali zilizokamatwa hapa zitataifishwa‘>>>Mkurugenzi wa Huduma wa Mamlaka, Gaudens Kayombo
Habari kutoka Clouds TV…CUF yaomba Suluhu umeya Tanga
Chama cha wananchi CUF kimeiomba Serikali kuingilia kati mgogoro wa Umeya unaoendelea katika Jiji la Tanga, ‘Mkurugenzi wakati anatangaza matokeo alitangaza tofauti na matokeo halisi, alimtangaza Rashid Jumbe wa CUF kuwa amepata kura 18 na Suleiman Mustapha wa CCM amepata kura 19‘>>>CUF
Habari kutoka TBC1.. Mkuu wa Mkoa amsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Hanang
Baadhi ya Madiwani wameupongeza uamuzi huu wa Serikali baada ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera Kumsimamisha Mkurugenzi wa almashauri ya Hanang kazi’, Ni kumuunga mkono Rais ambaye ni wewe mkuu wa mkoa kwamba haya mambo mengine ya ubaidhilifu wa mali za umma umeweza kuyatambua na kuyachukulia hatua‘>>>Diwani
Habari kutoka Star TV… Uhalifu KCMC
Mwanafunzi wa chuo cha KCMC kilichopo Moshi Kilimanjaro amechomwa na kitu chenye ncha kali na watu wanaosadikika ni vibaka,’Walikuja watu wakaniamsha lakini walinifichaficha mpaka tulipofika hospitalini ndio wakaniambia kuwa rafiki yangu amefariki‘>>>Rafiki wa Marehemu Justine
Habari kutoka ITV…Mamlaka Ya Maji Safi na Maji Taka
DAWASA yakamilisha ujenzi wa tanki linalohifadhi maji ya ujazo wa lita kumi
‘Hili ni nusu ya tanki hilo ambalo tumetenganisha tanki moja la duara lakini linatenganishwa na ukuta katikati, tunatenganisha hivi kwasababu tanki linavyoanza kufanya kazi likizeeka au tutakavyotaka kufanyia marekebisho tunaweza tukaamishia maji kwenye tanki lingine‘>>>Mkandarasi
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
BARABARA INAYOJENGWA KWA ZILE BILIONI 4 ZA SHEREHE ZA UHURU IMEFIKIA HAPA