Kama utakua ni mpenzi wa kutazama taarifa ya habari na hukupata time ya kutazama taarifa ya Habari April 26 2016 kupitia TV za Tanzania usijali millardayo.com imekurekodia habari 7 kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka Clouds TV…Muungano Bila Shamra Shamra
Leo April 26 ni maadhimisho ya sikuku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na siku ya leo hakujafanyika maadhimisho yeyote kama tulivyozoea miaka iliyopita……
>>>’katika maadhimisho kama haya hizi pesa zilikua zinapotea tu kwa kifupi zilikuwa zinaingia kwenye mifuko ya watu kwahiyo mimi namuunga mkono Rais Magufuli‘:- Mwananchi
Habari kutoka Clouds TV…CCP cha China Kuisaidia Tanzania
Chama cha kikomunisti cha China kimekubali kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania…… >>>’Wamenihakikishia kuwa China itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake na harakati zake za maendeleo‘:-Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
Habari kutoka ITV…Rungu la Magufuli Latua TCRA
>>>’Rais Magufuli ameivunja bodi ya Mamlaka na Mawasiliano ‘TCRA’ na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, taarifa iliyotolewa na Ikulu imeeleza kuwa sababu ya hatua hiyo ni wahusika kushindwa kusimamia mkataba wa utekelezaji uliosababisha hasara ya sh. bilioni 400 kwa mwaka‘;-Mwandishi wa habari
Habari kutoa Azam TWO…Kigamboni: Tupeni Usafiri Kupitia Darajani
Wakazi wa Kigamboni Jijini Dar es salaam wameiomba Serikali kuweka mazingira ya huduma ya usafiri utakaowarahisishia kuvuka kwenye Daraja la Nyerere …..>>>’Tulichokuwa tunaomba hasa sisi wakazi wa vijibweni ni Serikali kuweza kutulea vituo vya daladala kwenye hili daraja:- Mkazi
Habari kutoka Star TV…Ukwepaji Kodi na Ushuru
Mwenyekiti wa Makampuni ya Yono Stanley Kevela amesema mnada huo umeanza rasmi baada ya makampuni hayo kushindwa kulipa kodi…….>>>’kwahiyo mnada umeshafunguliwa na tutaendelea na ufilisi, sisi tutahakikisha kodi ya Serikali inalipwa na lengo la Seriakali ikusanye bilioni 18‘:- Stanley Kevela Mrugenzi Makampuni ya Yono
Habari kutoka ITV...Athari za Mvua
Zaidi ya ekari 10,000 za mashamba zimeharibika na mvua wilayani Pangani……….>>>’Yaani hapa pia mamba wamezaga hapa wako wakutosha yaani hata mifugo yetu inabidi kuiangalia wakati wa malisho‘:–Mkazi
Habari kutoka TBC1…Maslahi ya Pande Mbili za Muungano kulindwa na kuenziwa
>>>’Tumekubaliana kufikia mahali Tuweke kiwango maalumu cha idadi ya Wazanzibar watakaoajiriwa katika taasisi mbalimbali, kwahiyo tukafikia fomula hiyo ya asilimia 79‘:-Mohammed Aboud Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIIKOSA YA ZITTO KUHUSU UTUMBUAJI MAJIPU NA BUNGE KURUSHWA LIVE? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI