Habari zote zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya August 31 2016 usijali Millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano kubwa kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka Channel ten
Wavunja sheria ya katiba ya nchi kutovumiliwa
>>>‘kwa mujibu wa sheria hiyo nataka nitoe wito kwa wanasiasa kutii mamlaka ya sheria ya nchi yetu,na nataka nitoe wito kwa wananchi kutochochea au kuhamasishwa kuvunja sheria za nchi yetu kwa kujihusisha na mikusanyiko na maandamano ya aina yoyote ambayo imepigwa marufuku ikiwa kesho ama siku yeyote ile‘- Naibu waziri wa mambo ya ndani, Yusuf Masauni
Habari kutoka Clouds TV
Chadema yasitisha UKUTA
Katika kudumisha amani nchini ifikapo september mosi chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimesitisha mpango wake wa kufanya mandamano nchi nzima yaliyolenga kupinga udikteta nchini.
Habari kutoka ITV
Uhamiaji haramu
Uhamiaji kagera wamekamata wahamiaji haramu, wahamiaji hao ambao ni raia wa Uganda 86 watafuta vibarua bila kuwa na kibali nchini Tanzania.
Habari kutoka Azam TWO
CHADEMA tutalinda amani ya nchi
>>>’ Tuko tayari kufanya usafi na wanajeshi, tuko tayari kufanya lolote lakini kila jambo litakalo fanyika litakuwa ni kuhamasisha amani ya nchi hii‘- Mwenyekiti wa CHADEMA Ilemela, Greyson Warioba
Habari kutoka Clouds TV
Kuelekea miaka 52 ya JWTZ
JWTZ wamefanya huduma za kijamii ikiwemo kutoa huduma za afya bila malipoa na kufanya usafi wa mazingira .
ULIKOSA KUITAZAMA VIDEO YA SABABU ZA CHADEMA KUAHIRISHA UKUTA? UNAWEZA KUITAZAMA VIDEO NIMEKUWEKEA HAPA CHINI