Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya March 10 2016 usijali millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tisa kubwa kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka Channel 10…Watano Wafa Kwa Kufunikwa na Kifusi
Tukio hilo limetokea March 9 katika kata ya Mgusu Wilayani Geita, ‘Kabla ya kulipuka kwa mgodi ulianguka wenyewe, sasa kwa bahati mbaya kuna watu walikuwa tayari wako eneo lile wanafanya kazi ndio likawa limewateketeza, lakini baadhi ya watu walikimbia na wengine walijeruhiwa‘>>>Mchimbaji wa madini
Habari kutoka Channel 10….Wazee Wasiojiweza Kambi ya Salame
Wazee wasiojiweza wanaotunzwa katika kambi ya Salame iliyopo katika Wilaya ya Babati, Manyara wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa huduma muhimu kama chakula, umeme na magari. ‘Matibabu hapa ni shida usafiri hapa ni shida yaani kama wakati mwingine tunapanda pikipiki kama hauna pesa unapanda baiskeli‘>>>Mzee wa kituo cha Salame
‘Nikiwaangalia hawa wazee hapa kuna wengine wameshiriki hata vita vya pili vya Dunia hapa kuna wazee ambao wamepooza na wengine ni wagonjwa wamelala kitandani kama nilivyo waahidi, nitarudi tena niliende kuwashawishi Wanawake wenzangu tuje tuwasalimie wazee wetu‘>>>Anna Jideria Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara.
Habari kutoka Clouds TV…Rais Magufuli Atinga BOT
Rais Magufuli amewataka Wizara ya Fedha kufanya uhakiki wa Fedha wa malipo, ‘Tuashumu kwamba sasa hatuna deni hapa benki, wanarudi nyuma wakajipange upya , na wewe Waziri sasa uanze kufatili ya kwamba hili deni lina hitajika na hili haliitajiki hili tusije tukalipa madeni ambayo haya staili‘>>>Rais John Magufuli
Habari kutoka Clouds TV…Wadai Huduma ya Uhakika Kilombero
Baada ya kurejea kwa huduma ya Kivuko Wilayani Kilombero watumiaji wa kivuko hicho wameiomba Serikali kuhakikisha ujenzi wa daraja hilo unakamilika, ni baada ya shughuli za kiuchumi wa eneo hilo kuongezeka, ‘
‘Kivuko kinapokuwa hakifanyi kazi ujue wazi kuwa kule huduma za biashara zinakuwa zinatetereka hakuna kinachoendelea kwa kweli daraja hili ni muhimu kuliko watu wanvyoweza kufikiria‘>>>Mkazi wa Kilombero
Habari kutoka Azam TWO… Rais wa Vietnam Atembele EPZA
Rais wa Vietnum leo ameongozana na wafanyabiashara na kutembelea Makao Makuu ya Mamlaka ya Ukanda Maalamu EPZA, ‘
‘Tunataka maeneo yote yawe Special Economi Zone, wao wanasema wanazo Special Economic Zone 150 lakini kitu ambacho kimenipandisha pressure ni wanasema ukitaka kupata dola bilioni 20 kupitia Special Economic Zone unaweza kupata‘ Charles Mwijage Waziri wa Viwanda na Biashara
Habari kutoka ITV…Wananchi wavamia Makazi ya Familia ya Francis Nchobe na Kufanya Uharibifu
‘Wananchi hao wamefanya uharibifu baada ya kutuhumu Ukoo wa Familia hiyo kuhusika na kifo cha Ruben Emanuel Mkazi wa Kijiji cha Mgaduale ambaye mwili wake ulikutwa umetelekezwa kwenye moja ya shamba la mwana ukoo huo‘>>>Mwandishi wa Habari
Habari kutoka Star TV…Kuelekea Uchaguzi Mkuu Zanzibar
Akiongelea baadhi ya Mabalozi au Nchi kutotambua Uchaguzi huu ‘Sisi tuna katiba yetu tuna sheria zetu na utaratibu wetu tuliojiwekea kwahiyo kwasababu tunakiamini chombo chetu kitaendesha uchaguzi kwa haki na uhuru kwa hiyo hatuna wasiwasi nao wanavyoendesha shughuli zao za uchaguzi‘>>>Mohamed Aboud Mohamed Waziri ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
Habari kutoka Star TV…Kubenea Matatani
Mwanasheria wa Saed Kubenea, anadai ‘Polisi wanamshikilia Mteja wake kwa kosa la kumpiga Katibu Tawala na hata hivyo kutokana na Kubenea kukabiliwa na kesi nyingine katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kumtukana Mkuu wa Wilaya Kinondoni Paul Makonda ‘
Habari kutoka TBC1…Huduma zasitishwa kwa Muda Chumba cha Kuhifadhia Maiti Hopitali ya Tumbi,’
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Maendeleo ya Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla amekutana na mapungufu lukuki kwenye Hospitali ya Tumbi likiwemo tatizo la kukosekana maji safi na salama kwenye wodi ya Wazazi, ‘kutokana na hali hili Dr. Kigwangalla ametoa siku tatu kwa uongozi wa Hospitali ya Tumbi kufanya ukarabati kwenye chumba cha kuhifadhia Maiti.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTERFBYOUTUBE