Leo February 26, 2018 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekusudia kukata Rufaa kupinga hukumu iliyotolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya dhidi ya washtakiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ambaye pia alikuwa wakili upande wa utetezi Prof. Abdallah Safari amesema kuwa hawajaridhika na hukumu hiyo kwani hakuna sababu za msingi zilizopelekea washtakiwa hao kufungwa.
Prof. Safari amesema kuwa kwa sasa wamekwisha kukata rufaa na wanaomba dhamana ili wakati wa kusikiliza rufaa hiyo washtakiwa wawe nje ya kifungo.
FULL VIDEO: SUGU NA MASONGA WAKIPELEKWA GEREZANI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
BREAKING: SUGU ALIVYOFIKA MAHAKAMANI, UKAGUZI ULIOPO, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA