Miaka ya nyuma kidogo hususani kipindi ambacho simu za ‘smartphone’ hazikuwa nyingi, moja kati ya kampuni ya simu iliyojipatia umaarufu Duniani kote ni pamoja na Nokia.
Habari njema kwa wapenzi wa Teknolojia ni kuwa kampuni ya Nokia imetengeneza simu ya Android ambayo inadaiwa kuwa na ubora zaidi, kwani imetengenezwa kwa fremu ya chuma cha pua (stainless steel).
Simu hiyo inayojulikana kama Nokia 8 Sirocco itaingia rasmi sokoni mwezi April na itauzwa kwa Dola za Marekani 921 ambayo ni sawa na Tsh Milioni 2.2.
Inaelezwa kuwa chuma cha pua ambacho kinatengeneza fremu ya simu hiyo huifanya isiweze kuvunjika kwa mikono ya binadamu.
Polisi waongea kuhusu Maandamano yanayozungumzwa mitandaoni
BREAKING: Sugu ahukumiwa miezi mitano jela Mbeya