Leo February 17, 2018 zoezi la kupiga kura katika uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kinondoni limeanza ambapo wananchi wanapiga kura kumchagu Mbunge wa Jimbo hilo. Katika zoezi hilo Mgombe a Ubunge kwa tiketi ya CCM Maulid Mtulia ameongea baada ya kupiga kura .
Mtulia amesema atakubaliana na matokeo yoyote yatakayo tangazwa na Tume ya Uchaguzi Taifa pindi zoezi la kuhesabu kura litakapokamilika.
“Chama changu sio cha ulalamishi na hata kama kikiona hakikutendewa haki huwa kinafuata njia za kisheria kwa kufungua kesi Mahakamani kulalamikia matokeo lakini tutayakubali matokeo yeyote yatakayo kuja jioni” -Mtulia
‘KINONDONI TUTAFANYA BONGE LA COLLABO HAPA RUGE PALE DIAMOND’ MTULIA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA